Maendeleo ni nini?

Maendeleo ni nini?Dhana ya maendeleo iko kila mahali, katika maisha yetu binafsi, na katika maisha ya jamii na nchi kwa ujumla.
Sote tunaamini kuwa tunahitaji maendeleo,tusipofanya jitihada katika maendeleo, tunashinikizwa kwa namna moja au nyingine tufanye hiyo jitihada au tunaburuzwa tuendelee.
Katika kuziongelea nchi, watu hutumia dhana ya nchi zilizoendelea na nchi zinazoendelea au zisizoendelea,kwa mujibu wa dhana hizo, nchi kama Marekani, Uingereza, Sweden, Ujerumani, na Japani zinahesabiwa kuwa zimeendelea.
Lakini nchi kama Tanzania, Kenya, na Uganda zinahesabiwa kuwa nchi zinazoendelea,dhana hizi zimejengeka vichwani mwa watu, tangu zamani.
Je tunapotumia dhanahizi ,tunaelewa tunachoongelea?
Maendeleo ya jamii ni mchakato wa kujenga jamii endelevu,yenye kujiamini, kujituma na uwezo wa kushiriki,kwa misingi ya usawa na kuheshimiana, katika kubuni,kuandaa na kutekeleza mipango ya kujiletea “maendeleo” na kutumia matokeo ya kazi zao.
  • kuiwezesha jamii kutambua uwezo ilionao na kutumia raslimali zilizopo kutatua matatizo yao .
  • kuongeza ushiriki wa makundi yote katika jamii (wanawake, wanaume, watoto, wazee, vijana n.k) katika shughuli za maendeleo ili waweza kubuni na kuanzisha miradi ambayo ni endelevu na itakayowawezesha kujipatia au kujiongezea kipato kwa miradi iliyoanzishwa na mtu mmoja mmoja, kikundi au jamii kwa ujumla wao.
Wajasiriamaliwakiuza bidhaa sokoni
moja la soko almaarufu jijini Dar es salaam
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: