Kujiajiri ni chimbuko la mafanikio

KILA mwanadamu mwenye utashi thabiti huwa na kiu ya kufanya maendeleo kwenye sekta mbalimbali ili aweze kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya teknolojia, uchumi na utamaduni

Maendeleo ya familia na taifa, hayawezi kupatikana iwapo wananchi hawatashiriki kwenye shughuli za kujiongezea kipato ambazo ni halali.

Kwa muda mrefu watu wamekuwa na dhana kuwa kuajiriwa iwe serikali au kwenye sekta rasmi ndiyo msingi wa maendeleo lakini wanadharau kujiajiri ambako ndiko kwenye ajira nyingi zaidi.

Kuajiriwa na utegemezi ndivyo vinayowafanya walio na elimu kushindwa kuitumia ipasavyo pindi wanapokosa kazi za kuajiriwa huku wale wasio na elimu nao kujiona wanyonge, wasio na mwelekeo kwenye maisha yao.

Ni ukweli usiopingika kuwa iwapo watu wataelekeza nguvu zao katika kujiajiri taifa litapiga hatua kwenye maendeleo sambamba na kupunguza umaskini unaozidi kushamiri kadri siku zinavyokwenda.

Utegemezi nao kwa muda mrefu umekuwa ukichukua nafasi kwenye familia ambapo wanawake walionekana kuwa ni watu wa kufanya shughuli za nyumbani huku wakisubiri kuletea huduma na wanaume.

Dhana hiyo ndiyo ilijenga mazoeza kuwa kuna kazi zinazopaswa kufanywa na wanaume na mwingine za wanawake kwa kigezo kuwa ni ngumu na maalum kwa kundi fulan

Katika siku za hivi karibuni utegemezi huo unaonekana kuanza kuota mbawa hasa baada ya wanawake wengi kujiingiza katika shughuli mbalimbali za kujipatia kipato ikiwemo biashara, kilimo, uvuvi na nyinginezo.

Mabadiliko ya kiteknolojia, kukua kwa elimu na mwingiliano wa watu umechangia kwa kiasi kikubwa kuwakutanisha wanawake na kujiwekea mikakati ya maendeleo hasa kwa kujishughulisha na ujasiliamali.

wanawake wakiwezeshwa wanaweza

wanawake na maendeleo

Advertisements

2 Comments (+add yours?)

  1. Zainab Hemedy
    Oct 05, 2011 @ 14:53:47

    Ni kweli kujiajiri ni kuleta mafanikio.
    kwa sababu kama kila mtu akitegemea kuajiliwa na kusubili mshahara mwisho wa mwenzi utakuta anashindwa kufanya maendeleo mengine ya ziada ya haraka. kwasababu hanakuwa hana fedha ya kutosha ya kutatulia tatizo hilo kwa araka.Kwaiyo ni kweli kujiajili ni kuleta mafanikio nchini sio mafanikio binafsi tu.

    Reply

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: