maendeleo

Harusi za kibongo, ni kivutio kingine cha utalii japo zinazidi kutufanya tubaki maskini wa akili na maendeleo.

Hebu tufikirie kwa pamoja, kwa tukio la harusi tu unakusanya watu zaidi ya mia moja na watu wanachangia zaidi ya hata laki na kuendelea, lakini hawaangalia maendeleo yanakuwaje au wachangie kitu gani ili kuleta maendeleo katika nchi yao.

Katika mipango ya harusi hela nyingi zinatumika na wanapoteza millions za hela kwaajili ya kuchangia harusi ambayo ni ya siku moja.per night achilia mbali zilizokatikia kwenye vikao vya maandalizi. 

Mbwembwe ni nyingi zinafanya Harusi zionekane ni za kifalme, hata wageni waingiao nchini hujikuta wakishangaa kwa kutojua nini kinatokea na waambiwapo kuwa ni sherehe za harusi, hujikuta wakisikitika sana kwa kudanganywa kuwa Tanzania ni maskini wakati wanachokishuhudia ni tofauti.

Hivi jamani kwa nini kamati hizi za kijamii zisingekuwa kwa ajili ya maendeleo ya kielimu ya vijana wetu, kuongeza vifaa hospitalini, na maendeleo mengine katika jamii  milioni 25 tunazoziteketeza kwa tukio la siku moja tungekuwa tunazifanyia kazi ya maana Tanzania yetu ingefika mbali.


Misaada tunayoipata kutoka kwa nchi wafadhili ieleweke kuwa ni matokeo ya raia wa nchi hizo kuamua kujibana na kubadili mfumo wao wa maisha kimatumizi ili waweze kutusaidia sisi katika mambo mbali mbali ya kijamii. Kwanini sisi tunashindwa kufanya hivyo kwa ajili yetu wenyewe.


Kama kuna kitu kinaitwa kubana na kupunguza matumizi au matumizi yenye nindhamu basi na kianzie kwetu binafsi na ndani ya familia zetu, bila ya hivyo tabia hii itakua , kukomaa na kuwa sugu, na kujikuta na sisi bila ya kujijua tumejiandaa kwa muda mrefu kuwa aina fulani ya wafujaji ambao tunasubiri kugeuka kuwa mafisadi.


Tujiulize na kufanya maamuzi ya busura tuangalie vijana kwa maendeleo yetu na vizazi vijavyo ili waje wawe na maendeleo mazuri katika maisha yao ya baadae.


Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: