Tudumishe mila na utamaduni wa mavazi

Hali ya mvuto wa mfumo ya jamii wa Tanzania ni kivutio kikubwa kwa masuala ya utamaduni, uchumi na utalii.  Hadithi za watu wa kale, ngoma za asilia na aina ya ngoma zinatofautiana kati ya kabila na kabila.  Wanapocheza, Wamakonde kuchezesha viuno vyao kwenda sambamba na ngoma ya “sindimba”, Wazaramo humezwa na maandamano ya “mdundiko”.

Wamaasai huruka kwa mpangilio maalum huko wakitoa  sauti nzito ambazo zinaweza kumwogofya simba dume!  Matumizi ya nyoka hai na kucheza na nyoka wakubwa kama chatu kunakofanywa na Wasukuma wakati wanacheza ngoma ya “Bugobogobo” hakuwezi kusahaulika kwa mgeni. 

Kila kabila kati ya  makabila 120 ya Tanzania ina ngoma yake na staili zake za uchezaji ambazo zinapumbaza kwa kukazia macho zinafurahisha na kuvutia kijinsia.

Aina mbalimbali ya mavazi pia hutoa mvuto  wa aina yake kwa mgeni.  Wanaume wa Kimasai huvaa vazi ambalo halifuniki mwili wote huku wakitembea na mikuki, virungu na visu vikubwa.  Kwa upande wao, wanawake wa Kimasai hujaza tele shingo zao, mikono, miguu na masikio yao na vitu vya thamani vikiwemo shanga na hadi aina nyingine za madini.  Wanaume wa Kimasai hupakaza miili yao na udongo mwekundu uliochanganywa na mafuta yatokanayo na wanyama na husuka nywele zao

https://harusinamaendeleo.files.wordpress.com/2011/08/wamasai-1.jpg?w=300

wanawake wa kimasai

https://harusinamaendeleo.files.wordpress.com/2011/08/wamasai-4.jpg?w=300

wanaume wa kimasai

Wamakonde nao huchonga meno yao na kuchanja nyuso na miili yao taaluma inayotamanisha.  Wamakonde ni wataalam wa kuchonga vinyago vinavyoonyesha matatizo ya binadamu, mapambano, mapenzi, tamaa, wema, ubaya na mshikamano vitu ambavyo vinavutia sana na kuamsha fikra.

Makonde

katika maisha ya tanzania lazima tudumishe mila na utamaduni katika nchi yetu ili tuwe kivutio kizuri nje na ndani ya nji yetu ya tanzania kama jinsi wenzetu wamasai wanavyo fanya kudumisha mila na utamaduni ya kabila lao..


Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: