Uchumba wa wema na diamond platnam waleta gumzo

Licha ya kuwepo na furaha kubwa sana kutoka kwa muigizaji  mkongwe wa filamu za kibongo hapa nchini, Wema Sepetu kutokana na kile alichokizungumzia kuwa kama ndoto kwake baada ya kuvalishwa pete ya uchumba na msanii chipukizi wa muziki wa bongo flava, Diamond Platinum hatua hiyo bado imeacha gumzo ndani ya jamii mbalimbali.

Watu wengi kupitia vyombo vya habari mbalimbali wamekuwa wakihoji uhalali wa msanii huyo chipukizi kujihusisha kimapenzi na mwanamke ambaye amekuwa akikumbwa na kashfa mbalimbali ikiwemo ya kujihusisha kimapenzi na wasanii mbalimbali hapa nchini na pengine hadi kuchumbiwa zaidi ya mara mbili wakilinganisha na chipukizi huyo ambaye hata kiduchu hajakifikia kiwango cha Sepetu kimapenzi.

wakati mwingine gumzo nazo zilizidi mtaani huku watu wakihoji kwamba Diamond uamuzi alio uchukua wa kuwa na Wema, ni ushawishi toka kwa maswahiba zake, ama tamaa yakuwa na Wema kutokana na kwamba washakuwa katika mahusiano kwa kipindi kifupi,ama ni kuhitaji kuwa na mtu ambaye ni maarufu yaani {super star},kauli hiyo walikuwa wakiinyambua kutokana na watu ambao wema alishatembea nao,ambapo ikikumbukwa mtu wa mwisho hivi alikuwa naye ni mwigizaji mwenzake Stevine Kanumba,ambapo waligombana na   ikaleta gumzo na mwisho wa siku wakaachana,waswahili husema mfupa alio ushindwa fisi binadamu ataweza?

Akizungumza mmoja wa wakazi wa mji wa Dar es Salaam, Ibrahim Haji na pia anafuatilia kwaukaribu filamu za kibongo na historia za wasanii mbalimbali alionesha hisia zake huku akimsikitikia msanii Diamond akidai chaguo lake sio nzuri.

“Sidhani kama Diamond alipata ushauri wakutosha kutoka kwa watu wake wakaribu na pengine hakuomba kabisa ushauri'” alisema Bw. Hadji.

“Ni kweli kwamba Wema ni mwanamke mzuri na anastahili kuolewa lakini sio na mtu kama Diamond,amefanya matukio mengi sana kwa hiyo alistahili mtu wa aina yake,” aliongeza mkazi huyo.

Hata hivyo Bw. Haji alikataa kuweka wazi ni aina gani ya mume anayestahili kuoana na Wema na kusema si lazima ataje yeye bali ulimwengu unatambua kuwa Wema ni mojawapo ya mifupa aliyoushindwa Fisi.

wakati mwingine gumzo nazo zilizidi mtaani huku watu wakihoji kwamba diamond uamuzi alio uchukua wa kuwa na wema, ni ushawishi toka kwa maswaiba zake, ama tamaa yakuwa na wema kutokana na kwamba washakuwa katika mahusiano kwa kipindi kifupi,ama ni kuhitaji kuwa na mtu ambaye ni maarufu yaani {super star},kauli hiyo walikuwa wakiinyambua kutokana na watu ambao wema alishatembea nao,ambapo ikikumbukwa mtu wa mwisho hivi alikuwa naye ni mwigizaji mwenzake stevine kanumba,ambapo waligombana na  wakati mwingine ikaleta gumzo na mwisho wa siku wakaachana,waswahili husema mfupa alio ushinda fisi binadamu ataweza?

Siku chache baada ya Wema na Diamond kuchumbiana, walihojiwa na kituo fulani cha runinga hapa jijini,hali ambayo walionekana kutamba kwamba wanapendana,huku Wema akikiri kumpenda Diamond nakusema ni ngumu watu kuamini lakini ndivyo ilivyo,huku naye Diamond akionekana kuwa na furaha.

“Uamuzi wangu ndio huo na hilo ndilo chaguo langu na ninashangazwa na watu wengi kuona kama ni kitu cha ajabu mimi kuwa na Wema,”alisema Diamond.

Wema Sepetu alipata umaarufu mnamo mwaka 2006 aliposhnida taji la kisura wa Tanzania maarufu kama Miss Tanzania na baadaye kukumbwa na kashfa mbalimbali zikiwemo zile za ngono.Aliwahi kujihusisha kimapenzi na msanii mkongwe Steven Kanumba, Charles Baba na werngine wengi,kwa mujibu wa Bw. Hadji.

 

Advertisements

2 Comments (+add yours?)

 1. Zainab Hemedy
  Oct 05, 2011 @ 15:03:57

  Gumzo kivipi?alafu kama wewe ni mwanaharakati(mwana bloger wa harusi na maendeleo)unalichukuliaje suala zima la uvalishanaji waho wa pete sehemu kama club?au hamna sheria za muongozo wa utaratibu wa maandalizi ya harusi?

  Reply

  • mercey
   Oct 05, 2011 @ 15:10:57

   unajua nini dada zainabu,kilamtu na upangiliaj wake wa kumvalisha mpenzi wake pete,wahenga wanasema mapenzi ni kokote na akuna formula ya sehemu gani ya kuvalishana pete ata kwenye chini ya mti unaweza ukamvalisha….

   Reply

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: