Ndoa zinavyosababisha Wamasai kukeketwa

Wamasai, moja ya kabila nchini Tanzania linalosifika kulinda mila na desturi, hivi karibuni limeingia katika ulimwengu mpya baada ya moja ya mila zake inayotaka mwanamke kukeketwa kabla ya kuolewa kupigwa vita na wanaharakati wa haki za binadamu.

Kwa mujibu wa wanaharakati wanaopiga vita unyanyasaji wa jinsia mbalimbali wamesema kuwa kitendo kinachofanywa na jamii ya Kimasai kuwanyima haki ya kuolewa wanawake wasiokeketwa ni kwenda kinyume na historia zilizoko katika vitabu vyetu vya dini na pia kukiuka uumbaji wa mola wetu.

Historia ya vitabu mbali mbali vya dini na vya kimila, imeelezwa kuwa baada ya mwenyezi Mungu kuumba ulimwengu, aliweka kila kitu kinachopaswa kuwemo katika ulimwengu huo,na baada ya kuweka kila kitu akabakiwa na kazi ya kumuumba mwanadamu, ambaye historia inatuonyesha kuwa mwanaadamu wa kwanza kuumbwa alikuwa ni mwanaume, aliyefahamika kwa jina la Adam.

Baada ya kuumbwa binadamu huyo wa kwanza kazi ya uumbaji haikusimamia hapo baada ya muumbaji kuona kuna haja ya kumfanyia msaidizi wake huyo mwanaadam na ndipo alipoumbwa mama yetu hawa toka katika ubavu wa mumewe Adam.

Mfano huo wa kuumbwa kwa ulimwengu na hata kuonyesha umuhimu wa wanaadamu kuwa pamoja kama mume na mke kutokana na mada ninayotaka kuizungumzia hususan kwa upande wa ndoa hasa hizi za kimila katika jamii tofauti.

Kwa misingi  ya  kawaida za kidini,   ndoa  halali  ni  mapatano  ya  watu  wawili  wa jinsia  tofauti  wanaoamua kuishi  pamoja  kama  mume  na  mke  kwa ridhaa yao pasipo kulazimishwa na jamii inayowazunguka.

Hali hiyo ya kufuata taratibu za kidini na ridhaa ya muoaji na muolewaji ni tofauti kwa baadhi ya makabila katika kuendeleza ndoa hizo za kimila kwa kuwa wengi wanaamini suala la ndoa ni maamuzi ya upande mmoja.

Mfano wa jamii hiyo inayoamini ndoa ni ridhaa ya  upande mmoja ni wamaasai, kabila linalopatikana kaskazini mwa Tanzania  pamoja na sehemu ya nchi ya Kenya, kabila hili linaamini ndoa hasa kwa upande wa mwanamke ni ridhaa ya wazazi  wa binti.

Jamii hii inaamini ili binti aweze kuolewa ni lazima kwanza apitie hatua kadhaa ikiwemo suala la wazazi kumuelekeza kwa mume waliyekubaliana nae, ikiwa hiyo haitoshi ni lazima binti huyo apitie katika suala la kukeketwa kwa kile wanachoamini kuwa suala hilo litampunguzia matamanio na kumfanya atulie kwa mume .

Ingawa suala hili la kukeketa ni la hatari kwa afya nzima ya mwanamke  jamii hiyo haiwezi kumuamini binti ambaye hajapitia hatua hiyo na itabaki kumuona kama bado ni mtoto mdogo ambaye hawezi kuchangia jambo lolote katika jamii hiyo.

Mama Tarime anasema yeye ni mama mwenye umri wa miaka mingi, amekuwa mmoja wa akina mama wanaoendesha shughuli nzima ya kimila,hususani zile zinazomuhusu mwanamke kama vile masuala ya ndoa ingawa wana mipaka yao.

Anasema moja ya hatua muhimu ambayo mwanamke wa kimaasai anapaswa  kuipitia kabla hajaolewa ni suala la ukeketaji, ukeketaji kwa mujibu wa taratibu za kimaasai ni kitendo cha mwanamke kutoka katika hadhi ya utoto na kuwa mtu mzima,wanaamini  mwanamke anapokeketwa anaaminika kuwa anaweza kuwa jasiri katika masuala ya ndoa na ya kifamilia na ni heshima kubwa kufanyiwa tendo hilo..

“Mwanamke asipokeketwa anadharaulika,siyo na wanaume tu bali pia na wanawake wenzake kiasi kwamba anatengwa katika majukumu mengi ya kifamilia na kijamii bila kujali umri wake,kama haujakeketwa  wewe ni mtoto tu………. hata kama una umri mkubwa utadharaulika hata na wasichana wenzako na ndio maana suala la ukeketaji ni gumu kuliacha katika jamii yetu licha ya kelele zinazopigwa na wanaharakati mbalimbali” .

Anabainisha kuwa hata wanaume wa kimasai hawawezi kumuoa mwanamke ambaye hajakeketwa hali inayowafanya walio wengi kulazimika kuingia katika mtego huo kwa ajili ya kupata ndoa.

Ana Girsey mwanamke wa kimasai ambaye yupo katika ndoa kwa muda wa miaka minne sasa anasema katika mila zao  lazima msichana afuate utamaduni waliowekewa na wazee wao hata kama  jambo hilo ni la hatari,mwanamke aliyetahiriwa hupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa au wakati wa kujifungua hali inayopelekea wakati mwingine kutokwa na damu nyingi katika sehemu za siri

Kwa upande wake mtaalamu wa afya ya uzazi kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili Daktari, Asha Shabani anasema’

“ Wanawake waliotahiriwa wapo katika hatari kubwa ya kupoteza maisha wakati wa kujifungua kutokana na kuvuja kwa damu nyingi kunakosababishwa na makovu waliyopata wakati  wa kukeketwa, athari nyingine wanayoipata wanawake waliokeketwa ni kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kunakotokana na kutokujiamini kwa sababu ya mapungufu hayo yaliyosababishwa na mila hizo”.

Pia anasema kuwa wanawake wa aina hiyo wapo katika hatari kubwa ya kuwapoteza watoto wao wakati wa kujifungua kutokana na kukosa nguvu ya kusukuma kama ilivyo kwa wanawake wengine ambao hawajatahiriwa,hivyo suala zima la ndoa za kimasai ni chanzo kikubwa kinachosababisha ukeketaji kupamba moto kila siku.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: