Michango ya harusi

Harusi za kibongo, ni kivutio kingine cha utalii japo zinazidi kutufanya tubaki maskini wa akili na maendeleo.

Hebu tufikirie kwa pamoja, kwa tukio la harusi tu unakusanya watu zaidi ya mia moja na watu wanachangia zaidi ya hata laki na kuendelea, lakini hawaangalia maendeleo yanakuwaje au wachangie kitu gani ili kuleta maendeleo katika nchi yao.

Katika mipango ya harusi hela nyingi zinatumika na wanapoteza millions za hela kwaajili ya kuchangia harusi ambayo ni ya siku moja kwa siku, achilia mbali zilizokatikia kwenye vikao vya maandalizi. 

Mbwembwe ni nyingi zinafanya Harusi zionekane ni za kifalme, hata wageni waingiao nchini hujikuta wakishangaa kwa kutojua nini kinatokea na waambiwapo kuwa ni sherehe za harusi, hujikuta wakisikitika sana kwa kudanganywa kuwa Tanzania ni maskini wakati wanachokishuhudia ni tofauti.

Niliweza kuongea na mwanamama aitwaye Halima Bakari mkazi wa kijichi jijini Dar es salaam alisema kwamwezi huwa naletewa  kadi za mchango hata 3 au 4 na nilazima niweze kuchangia kwa muda unao itajika, na mimi nakuwa sina jinsi nilazima niweze kulipa kwasababu najua na mimi iko siku na mimi wanangu wataitajika kuolewa sasa nisipo wachangia majirani,marafiki atakae nichangia mimi siku yatakapo nikuta ni nani? Kwaiyo nakuwa najinyima ili niweze kuwachangia wenzangu, na hapohapo watoto wanatakiwa waende shule.

Mwanahamisi Amisi naye ni mwanadada ambaye yuko njiani kuolewa alisema,unajua unapokuwa katika jumuia ya watu unatakiwa kila kitu kitakacho kuwa kinatokea katika jamii ushirikiane nao,mambo yenyewe ni shida na raha,shida namaanisha misiba na matatizo mingine, raha ndio kamaizo harusi na sherehe zingine ukijifanya ndugu yangu wewe ndio mjuaji mambo yako yatakuwa yakipekeyako na familia yako,kwamfano bajeti ya harusi yako inakuja mamilion ya shilingi hiyo familia yako inaweza kuchangia hela zote izo haiwezekani kwaiyo ukiwa na ndugu,jamaa,marafiki wa kazini shughuli yako inaweza kuwa nzuri.

Unajua sio kwamba tunataka sana kulipa mishango ya harusi hapana maana uwezo haufanani,kwenye vikao vingine wanataka watu walipe kwaanzia elfu hamsini(50)na unaenda pekeyako, hapohapo majukumu ya nyumbani nayo yanakukabili,kuna ada,chakula bado haujawa na hela ya akiba hatakama pakitokea kitu hiyo hela ipo inaweza kukusaidia lakini inashindikana maana kila mwenzi lazima upate kadi ya mchango.

Kwamfano kama mimi mweziujao natarajia kuolewa kwaiyo natakiwa na mimi niwachangie wenzangu ili harusi yangu iwe ya ukweli naya kupendeza usipo lipa ya wenzio na wewe yakikufika hakuna kitu yani bora uchangie mchango na usiende kuliko ukakaa kimya.

 

Unajua katika maandalizi ya harusi unatakiwa wewe muoaji au wewe mwenyeshughuri uwe na hela ya kutosha ili uweze kufanikisha shuhuri yako na unapoita watu waje kwenye vikao wanatakiwa wakuchangie hela ndogo sana,lakini sio kwenye vikao vyetu mtu anaita kamati ukimuuliza unashilingi ngapi anaanza kujiuma uma oohh…ninaela kitogo ndio maana nimeitakikao kama tukiwa tunaendelea hivi tutakuwa tunalipa hela nyingi kwenye vikao vyetu na maendeleo yanazidi kuwa chini,alisema kijana huyo ajulikae kwa jina la Ali Hamisi mkazi wa Sinza

 

Hivi jamani kwa nini kamati hizi za kijamii zisingekuwa kwa ajili ya maendeleo ya kielimu ya vijana wetu, kuongeza vifaa hospitalini, na maendeleo mengine katika jamii  milioni 25 tunazoziteketeza kwa tukio la siku moja tungekuwa tunazifanyia kazi ya maana Tanzania yetu ingefika mbali.


Misaada tunayoipata kutoka kwa nchi wafadhili ieleweke kuwa ni matokeo ya raia wa nchi hizo kuamua kujibana na kubadili mfumo wao wa maisha kimatumizi ili waweze kutusaidia sisi katika mambo mbali mbali ya kijamii. Kwanini sisi tunashindwe kufanya hivyo kwa ajili yetu wenyewe.


Kama kuna kitu kinaitwa kubana na kupunguza matumizi au matumizi yenye nindhamu basi na kianzie kwetu binafsi na ndani ya familia zetu, bila ya hivyo tabia hii itakua , kukomaa na kuwa sugu, na kujikuta na sisi bila ya kujijua tumejiandaa kwa muda mrefu kuwa aina fulani ya wafujaji ambao tunasubiri kugeuka kuwa mafisadi.

Tujiulize na kufanya maamuzi ya busura tuangalie vijana kwa maendeleo yetu na vizazi vijavyo ili waje wawe na maendeleo mazuri katika maisha yao ya baadae.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: